Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Njia ya kuelekea Karbala, siyo safari ya mpito, bali ni kuinuka Kiroho daima.
Na kila anayeitembea, huandika mstari usiofutika katika ukurasa wa mapenzi ya kweli na ashiki ya Imam Hussein (as).
Kwa ibara nyingine: Safari ya Ziara ya Karbala si Mwendo tu, Bali ni Maandishi ya Upendo wa Milele kwa Imam Hussein (as) - Mjukuu Kipenzi wa Mtume Muhammad (s.a.w.w). Ni njia inayounganisha safari na Ukurasa wa ashiki isiyofutika.
Aidha, njia hiyo ya safari ya Arubaini katika Ardhi ya Karbala, inatengeneza Ukaribu wa Kiroho na Hussein (a.s) Katika Kila Hatua unayoipiga ukielekea kumzuru Aba Abdillah Al-Hussein (as).
Your Comment